Mkuu wa Mawasiliano Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Innocent Mungy akizungumza katika bonanza
hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
…………………………………………………………………….
Na Hassan Silayo
Zaidi ya wananchi 500 wakiwemo
waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano Serikalini wamepima afya
katika bonanza lililoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano
serikalini, jukwaa la wahariri na klabu ya waandishi Dar es Salaam.
Bonanza hilo lililohusisha pia
uchangiaji damu kwa hiari na ufanyaji mazoezi ya viungo ili kuunga mkono
agizo la Makamu wa Rais Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan ili
kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Akiongea mara baada ya kupima
afya Sharifa Hussein mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam amesema kuwa
anawapongeza waliofanya uratibu wa kupeleka madaktari kwani imewapa
fursa ya kujua hali za afya yao pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.
“Niliona tangazo kuhusu upimaji
afya hapa, nimekuja nimepima nimepata majibu pamoja na ushauri, kwakweli
nawashukuru waandaaji wa shughuli hii, imesaidia wengi kujua hali za
afya zao na sasa ni jukumu letu kwenda kufanyia kazi yale tuliyoambiwa
baada ya mati Watoto Alisema Bi.Sharifa.
Akiongea baada ya kumaliza
programu ya mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja mkurugenzi mkuu wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa
watanzania hawana budi kufanya mazoezi mara kwa mara kwani inasaidia
kupunguza gharama zinazoweza kutumika kutibu magonjwa yanayoweza
kusababishwa na kutofanya mazoezi ambayo yamekuwa yakisumbua wengi hasa
gharama za matibabu yake.
Naye Mwenyekiti wa Chama
chaMaafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy amesema
kuwa wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuunga mkono agizo la makamu wa
rais makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ili
kujikinga na magonjwa yasiyoambuka.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri
(TEF) Teophil Makunga aliwasisitiza wanannchi kuweka programu binafsi za
kufanya mazoezi kwani mazoezi yana saidia kupunguza uwezekano wa kupata
magonjwa mara kwa mara pia yanasadia kufikiri na kufanya mambo vizuri.
Mratibu wa Magonjwa
Yasiyoambukizwa Dkt Digna Siriwa Alisema kuwa kutokana na ripoti
iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) alisema kuwa kwa mwaka
2008 asilimia 63 ya watu ulimwenguni walikufa kwa mgonjwa
yasiyoambukizwa ikiwemo Presha, Sukari, Kansa pamoja na magonjwa ya
mfuko wa hewa ambayo yanaweza kuzuiwa kwa kufanya mazoezi
Bonanza hilo limeandaliwa na
Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini, Jukwaa la Wahariri, Klabu ya
Waandishi wa habari wa Dar es salaam pamoja na kuratibiwa na Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.


0 comments :
Post a Comment