Baada ya mchezo wa katika ya wiki dhidi ya PSG ,FC Barcelona hapo kesho itakua na kibarua kizito pale itakaposafiri na kuelekea Galicia kuikabili Daportivo ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu nchini Hispania na dhumuni kubwa ni kupata pointi 3 muhimu ili kuzidi kujiweka mbeke zaidi ya wapinzani wao Real Madrid.
Katika michezo mitano ya mwisho kuzikutanisha timu hizi Barcelona imeshinda michezo mitatu ikiwemo ule wa goli 8-0 katika uwanja wa Deportivo huku zikitoa sare mara mbili na Deportivo hajashinda mchezo wowote.
Hata hivyo Barcelona itawakosa Alex Vidal na Jérémy Mathieu katika mchezo utakaofanyika hapo kesho.
0 comments :
Post a Comment