BAADA ya wakazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam jana kuachwa na vilio wakati Kampuni ya Rasilimali za Shirika la Reli Tanzania (RAHCO) ilipoendeleza zoezi la kubomoa nyumba zilizokuwa katika eneo la hifadhi ya reli, moja wa wamiliki wa maeneo makubwa sehemu hiyo, Sali Said Bakhresa apewa siku kumi kuboa ukuta ambao umo katika eneo la Reli.
RAHCO iliendesha zoezi hilo ilikuwa ikibomoa nyumba zilizokuwa zimejengwa katika hifadhi ya reli ambayo ni mita 30 . Zaidi ya nyumba 250 zilibomolewa jana.
Akizungumza jana, Ofisa Uhusiano wa RAHCO, Catherine Moshi, alisema kuwa wakazi wa eneo hilo walipewa notisi ya kwanza Aprili mwaka jana wakitakiwa kuhama eneo hilo, lakini wakakumbushwa tena Julai mwaka huohuo.
Baada ya kuona kuna ambao hawajahama, walipewa tena notisi ya kuwakumbusha Februari mwaka huu kabla ya zoezi la kubomoa kuanza hapo jana
0 comments :
Post a Comment