KIKAO cha kamati ya Utendaji ya Yanga kilichokaa asubuhi ya leo kimemalizika muda mfupi uliopita na kutoka na maamuzi ya kuachana na mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo, Hans Pluijm.
Habari zilizotufikia toka chanzo chetu klabuni hapo zinasema baada ya msuguano wa muda mrefu hatimaye wajumbe hao waliafikiana kwa kauli moja kumfuta kazi Pluijm huku ikishindwa kuwekwa wazi sababu za uamuzi huo.
Pluijm alikuwa kocha mkuu wa Yanga kabla hajaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mzambia George Lwandamina.



0 comments :
Post a Comment