KUHUSU ELIMU YAKE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefunguka tuhuma
zinazozushwa kupitia mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kuhusu elimu
yake na zinazoeleza kuwa amefoji cheti cha mtu mwingine.
Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) RC Makonda
ameeleza kuwa kinachogombaniwa siyo Makonda bali ni kiti alichokalia
(UKUU WA MKOA), hivyo ameeleza kuwa nafasi yake ya ukuu wa Mkoa amepewa
na Mungu.
Na kufafanua kuwa hatakama angepata sifuri au daraja la kwanza katika
masomo yake, Mungu angetaka awe Mkuu wa Mkoa angekuwa tu, kwani Mungu
ndiye anapanga kila kitu na kuongeza kuwa yupo imara kuliko alivyokuwa
jana.
KUTISHWA KWA WAZAZI WAKE
Pia RC Makonda amefunguka kuhusu kutishwa kwa baba yake mzazi, pia kuna
watu walikwenda eneo analoishi baba yake na mama yake mzazi na kupiga
picha, ili wakaoneshe nyumba anayoishi mzazi wake.
KUHUSU KUITWA SHOGA NA MGUMBA
RC Makonda ameeleza kuwa watu wamekuwa wakimtolea lugha chafu kuhusu
uzazi wake na kumuita mgumba kwa kuwa hana mtoto na wengine wamekuwa
wakimuita shoga, amefunguka na kusema kuwa haoni tusi jipya.
RC Makonda amesema ipo siku watu wataulizwa kuhusu matendo wanayoyafanya
duniani kilasiku, hawana budi kuwa makini na matendo yao.
KUHUSU DAWA ZA KULEVYA



0 comments :
Post a Comment