Kulikuwa na hisia kali katika bunge la Israel siku ya Jumatano wakati lilipopitisha sheria kuzuia vipaza sauti miongoni mwa taasisi za kidini.
Baadhi ya wabunge Waarabu walizikatakata baadhi ya nakala za muswada huo wakati wa mjadala.
Muswada huo utalazimika kusomwa kwa mara nyengine na kupitishwa kabla ya kufanywa sheria.
Toleo moja la muswada huo linapiga marufuku taasisi zote za kidini kutumia vipaza sauti kati ya saa tano na saa moja.
Toleo jingine linapiga marufuku vipaza sauti vinavyoonekana kuwa na kelele zaidi muda wowote wa siku.
Ni marekebisho ya muswada ulioidhinishwa na baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu mnamo mwezi Novemba.
Bwana Netanyahu alisema kuwa amepokea malalamishi kadhaa utoka katika jamii zote za Israel kuhusu kelele na matatizo wanayopata kutokana na kelele hizo zinazotoka katika vipaza sauti.
Mmoja ya watu wanaopigia debe muswada huo Motti Yogev wa chama cha Jewish Home Party alisema siku ya Jumatano kwamba ni muswada unaolenga kuwasaidia raia kupumzika
''Hatuna nia ya kuwaumiza wafuasi wa dini yoyote'', aliongezea.
Wakosoaji wa muswada huo wanasema kuwa unakandamiza uhuru wa kuabudu.
''Sauti ya ''Adhan'' haijawahi kusababisha uchafuzi wowote wa mazingira.Ni mojawapo ya tamaduni za dini ya kiislamu na hatujawahi kingilia sherehe yoyote ya kidini inayohusu Judaism. Vitendo vyenu ni vya kibaguzi'' ,alionya Ahmed Tibi wa chama cha Joint List alliance chenye Waarabu wengi.
''Hatua hii inalenga Uislamu'', aliongezea.
Ayman Odeh kiongozi wa muungano huo alifurushwa nje baada ya kukatakata nakala ya muswada huo.
Netanyahu ataka sauti za 'adhan' kupunguzwa misikitini
Raia wa Kiarabu nchini Israel wanaojulikana kama Waarabu Waisraeli ni kizazi cha Wapalestina 160,000 waliosalia baada ya taifa la Israel kubuniwa 1984.
Wao ni asilimia 20 ya idadi ya Waisraeli .
Asilimia themanini ya Waisraeli Waarabu ni Waislamu na waliosalia wamegawanyika sawa kati ya Wakristo na Druze
chanzo
bbcswahili
0 comments :
Post a Comment