Kesi Ya Madai Cuf Kutajwa Mwezi Ujao

Wanachama nane wa chama cha CUF, akiwemo mbunge wa Jimbo la Kaliua Tabora, Magdalena Sakaya Leo wamewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya madai iliyofunguliwa na bodi ya wadhamini ya CUF

Pingamizi hilo la awali  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa wadaiwa, Mashaka Ngole na litasikilizwa Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri.

Katika pingamizi hilo, wakili Ngole anadai kuwa, maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Bodi ya wadhamini ya CUF kupitia Wakili Hashimu Mziray hayawezi kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Amedai kuwa maombi hayo yanashughulikiwa katika maombi namba 23 ya 2016 yaliyopo Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam.

Ngole ameendelea kudai kuwa, muombaji hana mguu wa kusimamia kufungua kesi dhidi ya wajibu maombi na kwamba maombi hayo hayana msingi kwa sababu yameshindwa kubainisha jina la mwandishi wa masula ya fedha.

Aidha wameomba mahakama itupilie mbali maombi hayo kwa gharama.Kufuatia pingamizi hilo, wakili Mziray aliiomba mahakama iwapatie muda wa kujibu pingamizi hilo kwa kuwa walikwisha patiwa nakala ya pingamizi hilo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 12 mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza pingamizi hilo. Kesi ya msingi imepangwa kutajwa Mei 8,2017.

Awali, Bodi ya wadhamini ya CUF, kupitia wakili Mziray ilifungua kesi ya madai mahakamani hapo ikiomba zuio la muda ili Sakaya na wenzake saba wasiweze kujihusisha na uongozi wa chama na kufanya mikutano na waliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura.

Katika maombi hayo iliyofunguliwa chini ya hati ya dharula, wajibu maombi ni Magdalena Sakaya na wenzake Thomas Malima, Maftah Nachumu, Omar Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.

Katika maombi ya bodi ya wadhamini wanaiomba mahakama itoe zuio la muda kwa kuwazuia wajibu maombi ama mawakala wao au watu wao kujihusisha katika masuala yoyote ya uongozi ama kufanya mikutano ya chama hicho,  hadi maombi yatakaposikilizwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment