Manfongo Afunguka Sababu Yakutotoa Wimbo Wake Mpya


Msanii wa singeli, Manfongo amesema yeye kushindwa kuachia wimbo wake aliomshirikisha Mr Blue ni kwa sababu ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kumtaja Blue katika orodha ya watu wanaojihusisha na matumizi  ya dawa za kulevya.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz cha EATV, Manfongo amesema kuwa wimbo huo ulikuwa katika maandalizi  mazuri lakini baada ya kusikia jina la Blue katika watu walioambiwa wahudhurie kituo cha polisi akaona ni afadhali kwanza amuache msanii huyo amalize matatizo yanayomkabili kwanza.

“Blue alinipigia simu akanambia mdogo wangu nimepata ‘show’ Muscat  si unajua familia lazima ile? sasa ameondoka tu Mkuu wa Mkoa naye  akatangaza majina ya watu anaowataka kufika kituo cha polisi naye akawepo.  Nikaona kwa vile mashabiki walikuwa wanajua ujio wa kazi yangu mpya bora niachie hii ‘Safi tuu’ halafu kichwa cha kaka yangu kikitulia tumalizie kazi  lakini mashabiki wanachotakiwa kujua ni kuwa kazi hiyo ipo na lazima tuitoe".- alisema Manifongo

Katika hatua nyingine Manfongo amesema yeye kuacha kufanya kazi na meneja wake wa zamani G-Maker siyo kwamba ndiyo muziki wake utakuwa umekufa bali ndiyo atakaza kufika kimataifa kwani yeye ndiye mwenye muziki huo.

Kwa sasa Manfongo anasimamiwa katika kazi zake na Wasowiso ambaye ni meneja wake wa zamani ambapo amesema atatumia pesa zake kuji- 'brand' na siyo kuwapa watu hela waliokuwa wanamtumia bila faida.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment