Kiungo mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva atafanikiwa kuvunja rekodi yake aliyoiweka msimu wa 2014/15? Katika msimu huo Msuva alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga jumla ya magoli 17 ambayo yaliisaidia Yanga kushinda taji la ligi katika msimu huo chini ya kocha Hans van Pluijm.
Sasa hivi msuva amefikisha magoli 12 kwenye ligi zikiwa zimesalia mechi saba (sawa na dakika 630) ili ligi ifikie ungingoni, Msuva anahitaji magoli matano (5) zaidi ili aweze kuifikia rekodi aliyoiweka msimu wa 2014/15 wakati anashinda tuzo ya ufungaji bora. Anahitaji magoli sita au zaidi ili kuivunja rekodi yake mwenyewe, je kwa kiwango alichonacho sasa, anaweza kufikia rekodi yake na kuivunja?
Katika msimu huohuo (2014/15) Msuva alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi (VPL) kwa kuwashinda waliokuwa wapinzani wake msimu huo kwenye category hiyo (Mrisho Ngasa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’).
Katika msimu huu ambao unaelekea ukingoni, Msuva amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu kuanza kwa msimu, anafunga na kutengeneza magoli kadiri awezavyo, lakini pia ameonesha kiwango kizuri kwenye mechi nyingi alizoitumikia Yanga kuanzia ligi kuu, Azam Sports Federation Cup (FA Cup) na mashindano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.
Msimu uliopita hakufanikiwa kuchua tuzo yoyote, ambapo tuzo alizokuwa akizishikilia zilikwenda kwa wachezaji wenzake wa Yanga (mfungaji bora ilichukuliwa na Amis Tambwe huku ile ya mchezaji bora ikienda kwa beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul).
Msuva bado yupo kwenye presha ya kuibuka mfungaji bora kutokana na wanaomfuta nyuma yake kutenganishwa na gape dogo la magoli. Kichuya ana amagoli 10, Tambwe mshindi wa tuzo hiyo msimu uliopita ana magoli 9 uku wachezaji wengine wanne wakiwa nyuma kila mmoja akiwa na magoli nane.
Kwa mazingira hayo, Msuva ataweza kufikia na kuivunja rekodi yake mwenyewe ya msimu wa 2014/15?

About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :
Post a Comment