Mwalimu Akamatwa Na Viroba Vya Mamilioni Igunga


MWALIMU wa shule ya sekondari ya St Margareth wilayani Igunga amekamatwa na boksi za pombe aina ya viroba 825 akiwa amevihifadhi katika duka lake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani alimtaja mwalimu aliyekamatwa na maboksi hayo kuwa ni John Pastory (48).

Kamanda Selemani alisema mwalimu huyo alikamatwa Machi 7, majira ya saa 5 asubuhi katika mtaa wa Mwayunge mjini Igunga.

Alisema baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata vioroba hivyo vyenye thamani ya sh 77,136,000.

Aidha kamanda Selemani alisema mwalimu huyo ndiye alikuwa msambazaji mkubwa wa pombe aina ya viroba wilaya ya Igunga.

Nae mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwayunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Abel Shampinga alilipongeza jeshi polisi kwa kuwakamata wauzaji wa pombe za viroba na kuongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwayunge hayuko tayari kuwatetea watu wanaovunja sheria za nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment