Sababu Ya Magufuli Kutomtumbua Makonda Hadi Sasa

Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.
Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.
Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.
Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.
Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.
Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.
Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.
Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.
Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.
Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?
Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyonyo zenu? Acheni masikhara bana.
Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
SOURCE:JF
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment