Simba Yaweka Mikakati Ya Kuchukua Ubingwa Ligi Kuu



SIMBA wamepiga hesabu wakishinda mechi tatu za Kanda ya Ziwa watakuwa wameipiga bao Yanga katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mechi hizo zinazohusisha timu za kanda hiyo, kwa vyovyote Simba wakifanikiwa kushinda zote watakuwa wamepata pointi tisa ambazo zitawaweka katika mazingira bora zaidi ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Kwa kutambua umuhimu wa mechi hiyo, Simba wameweka mikakati kabambe itakayowawezesha kuibuka na ushindi, ikizingatia Yanga wana mechi pia na timu hizo za Kanda ya Ziwa ingawa Yanga watecheza mechi mbili Dar es Salaam.

Simba ikiwa Kanda ya Ziwa itacheza na Toto Africans, Mbao na Kagera Sugar na baadaye watarejea jijini Dar es Salaam kucheza na African Lyon, Mwadui na Stand United.

“Tumegundua kwamba Yanga watakwenda kucheza na Mbao, hivyo sisi kwa namna yoyote tunataka kuwatia hasira Mbao ili Yanga wakiingia huko wabakishe pointi na kuwawahi Mbao ni kuwafunga tu ili wakae sehemu ngumu kwenye ligi kisha hasira zao watazimalizia kwa Yanga,” alisema Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’.

Hesabu za Simba kama zitatimia kwa kuifunga Mbao na Toto Africans, maana yake ni kwamba timu hizo zitakuwa kwenye mazingira mabaya zaidi kwani hadi sasa Mbao iko nafasi ya 12 ikiwa na pointi  27 wakati Toto Africans iko katika nafasi ya  14 ikiwa na pointi  27 hivyo timu hizo kufungwa na Simba zitakuwa pabaya zaidi.

Habari za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya Simba zilisema kwamba, viongozi wa klabu hiyo wameunda kamati maalumu itakayofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanapata pointi zote za Kanda ya Ziwa na kuacha msala mkubwa kwa Yanga.

Mtoa habari wetu mwingine mbali na Meneja wa Simba ambaye hata hivyo aliomba tumhifadhi jina alisema kwamba, kamati hiyo maalumu inaundwa na vigogo ambao wanazijua fitina za soka.

Alisema viongozi wa Simba wamelazimika kuunda kamati hiyo kutokana na ugumu wa mechi za Kanda ya Ziwa.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, amekiri kuwepo kwa mikakati ya kuhakikisha wanapata pointi tisa kwa mechi tatu watakazocheza Kanda ya Ziwa.

Mayanja alisema mechi hizo ni muhimu kwao kushinda kwani zitatoa jibu la wao kuchukua ubingwa msimu huu, baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment