Viongozi Wa Chadema Waliohukumiwa Miezi NaneJela Waachiliwa Kwa Dhamana


Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Lindi Suleiman Mathew pamoja na katibu wa tawi la chama hicho kata ya Nyamangala Ismail Kapulila waliohukumiwa kifungo cha miezi nane jela kila mmoja kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja  na mahakama kuu kanda ya Mtwara.



Mnamo January 18 mwaka huu mahakama  ya mkoa wa Lindi ilimtia hatiani mwenyeki wa CHADEMA mkoa wa Lindi Suleiman Mathew pamoja na katibu wa chama hicho tawi la Nyamangala Lindi Ismail Kapulila kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.


Hata hivyo baada jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo Lameck Mikael kupitia maombi ya watuhumiwa  aliona hakuna kipingamizi chochote cha kuwanyima dhamana



Kesi hiyo ambayo ilionyesha kuvuta hisia za wafuasi wa CHADEMA kutoka mkoa wa Mtwara na Lindi huku wakiongozwa na katibu mkuu  taifa wa chama hicho Dr Joseph Mashinji  anazungumza haya  nje ya mahakama.



Hata hivyo watuhumiwa wanaomba kesi ya msingi ya rufaa no 11 ya mwaka 2017 wanapinga kutiwa kwao hatiani na kuiomba mahakama kuondoa shauri hilo.



Watuhumiwa wanatakiwa kuripoti mahakamani kila juma la kwanza la mwezi, na kesi ya msingi itatajwa tarehe 3-5-2017.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment