Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn kwenda kuangalia vikundi vya ngoma za asili kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kurejea nchini kwake mara bada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn kabla ya kupanda ndege na kuondoka jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakijadiliana jambo mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuchangia vikundi mbalimbali vilivyotumbuiza uwanjani wapo wakati wageni mbalimbali wanapowasili kiasi cha Tsh. Milioni 15 kama kuthamini mchango wao wanaoutoa. Pia Waziri Mkuu Majaliwa aliwachangia kiasi cha Tsh. Milioni 5. Wakwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar
0 comments :
Post a Comment