Simon Sirro amedai uhalifu nchini unaweza kupungua kama kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi la polisi nchini sababu wahalifu hao wanaishi katika jamii zetu hizi hizi.
“Kipaumbele kikubwa ni uhalifu hivyo kazi yangu ni kuhakikisha uhalifu unapungua kwa kiasi kikubwa ili Watanzania waishi kwa amani lakini uhalifu huu utapungua tukipata ushirikiano mzuri na jamii, sababu hao wahalifu wanaishi kwenye jamii kwa hiyo ombi langu kwa Watanzania ili waishi kwa amani na utulivu ni vizuri sana watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi. Naamini kabisa tutaweza sababu hawa wahalifu ni wachache kuliko sisi kwa hiyo umoja wetu ule lazima tutashinda” alisema Sirro

Mbali na hilo IGP Sirro ametoa onyo kwa wahalifu wote nchini akiwataka waache mara moja kwani mwisho wa siku watapoteza tu maisha yao na kuacha familia zao zikipata shida.
“Lakini niwape onyo wahalifu kuwa uhalifu haulipi, kung’ang’ania uhalifu mwisho wa siku utaacha familia yako hivyo ni afadhali ufanye kazi ya halali itakusaidia kulea familia yako lakini ukijiingiza kwenye uhalifu wa ujanja ujanja haitakusaidia kitu, mwisho utaacha familia yako” alisisitiza IGP Sirro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Mei, 2017 amemuapisha Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).
Hafla ya kuapishwa kwa IGP Simon Nyakoro Sirro imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson John Mdemu, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Makatibu Wakuu wa Wizara na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Paul Christian Makonda.
Kabla ya IGP Simon Nyakoro Sirro kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mhe. Rais Magufuli amemvua cheo cha zamani cha Kamishna wa Polisi na kumvalisha cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Polisi.
Katika hafla hiyo IGP Simon Nyakoro Sirro, pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Utumishi wa Umma kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. John Marko Kaole.
IGP Simon Nyakoro Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine

0 comments :
Post a Comment