Klabu ya Singida united imezidi kujiimarisha kwa kuelekea msimu ujao wa ligi kuu kwa kuongeza nguvu katika kikosi chao, mastaa wengi wenye majina makubwa wameongezwa katika timu hiyo.
Singida United ambao leo wameanza rasmi mazoezi katika uwanja wa Uhuru chini ya kocha wao mpya Hans Van Pluijm na msaidizi wake Fred Felix Minziro wamekiongoza kikosi vyema kujiandaa na mashindano ya SportPesa Super Cup hali kadhalika ligi kuu.
Deus Kaseke kutoka Yanga Ndiyo ingizo jipya la kocha Hans Van Pluijm na anatarajiwa kuripoti mazoezini kesho pamoja na Kenny Ally mwambungu aliesaini singida United siku chache zilizopita kwa ada ya shilingi Milioni 30
0 comments :
Post a Comment