BARUA TOKA TAMISEMI
Ipo taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakiwemo makundi yaWhatsApp’, ‘Facebook’ na majukwaa mbalimbali ikiwataka waombaji wa ajira za ualimu kuomba ajira hizo kupitia anuani za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ambazo ni simu 026-2322848, barua
pepe ps@tamisemi.go.tz na kupitia mfumo wa ONLINE TEACHERS EMPLOYMENT
APPLICATION SYSTEM (OTEAS) jambo ambalo halina ukweli.
Taarifa hii imekuwa ikijirudia rudia na tumekuwa tukiikanusha mara kwa mara kupitiamitandao ya kijamii lakini kila baada ya muda fulani imekuwa kisambazwa upya kama taarifa mpya na kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaosubiri kuomba ajira za ualimu.
Tunapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa hakuna tangazo la kukaribisha maombi ya ajira za ualimu lililotolewa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI hivi karibuni na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuomba nafasi hizo kupitia anuani za Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwakuwa hatujatangazakuwepo kwa nafasi hizo.Ofisi ya Rais – TAMISEMI inaendelea kuwasihi Watanzania kuwa makini na matangazo ya uzushi katika mitandao mbalimbali ya kijamii yanayopelekea kutapeliwa.
Matangazo halisi yanayotolewa na Ofisi yRais-TAMISEMIyanapatikana kupitia tovuti ya OR TAMISEMI ambayo niwww.tamisemi.go.tz.Pia waweza isoma barua yenyewe iliyotolewa na TAMISEMI hapo chini