Klabu ya Toto Africans ya Jijini Mwanza imetoa ruksa kwa mchezaji wake yeyote ambaye atapata timu nyingine ya kuchezea katika msimu ujao kuwa huru kuondoka.
Hatua hiyo imekuja baada ya kikosi cha timu hiyo kuanza kuondokewa na wachezaji wake muhimu kwa kusajiliwa na vilabu vikubwa nchini vya Simba na Azam.
Wachezaji waliondoka katika klabu hiyo ni mshambuliaji,Waziri Junior, aliyekwenda Azam FC na Yusuph Mlipili aliyesajiliwa Simba SC, huku wengine wakiendelea kuwindwa.
Mwenyekiti wa timu hiyo Godwin Aiko amesema kuchukuliwa kwa wachezaji wao hakutaiyumbisha timu hiyo kwakuwa wana timu nzuri za vijana na kujigamba kuwa Toto Africans ni chuo cha soka na ndiyo sababu ya kuwindwa na vilabu vikubwa.
“Sisi ni kama chuo, wao waje tu wawachukue, sisi hatuishiwi na wachezaji yeyote atakayepata nafasi kwenye timu yoyote aende, hatuwezi kumzuia maana hiyo ndiyo njia ya mafanikio yake, na sisi tunapenda vijana wafanikiwe” Amesema Aiko
0 comments :
Post a Comment