Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Lesotho, Kocha Mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga ameahidi kutumia michezo iliyosalia kusahihisha makosa yaliyofanywa na wachezaji wake katika mchezo huo uliopigwa jana usiku.
Mayanga amesema mabeki wa Taifa Stars walifanya makosa ya kushindwa kulinda bao lililopatikana kupitia kwa nahodha Mbwana Samatta, na kupelekea vijana hao wa Lesotho kusawazisha, na kisha kucheza mchezo wa kujilinda zaidi
Mbali na kuwapongeza Lesotho kwa kuweza kujilinda, pia Mayanga amesewatupia lawama wachezaji wake kwa kushindwa kutumia nafasi kadhaa zilizotengenezwa huku akikiri kuwa walikuwa wakiichukulia Lesotho kama timu dhaifu.
“Hakuna timu kibonde kwenye mashindano…. Wenzetu walikuja na mbinu, na mpira ni mchezo wa mbinu, tayari tumepoteza pointi 2 kati ya 9 za nyumbani lakini tunaamini katika pointi 7 za nyumbani zilizobaki tutapigana kuona nini cha kufanya….” Amesema Mayanga
Kwa upande wake Kocha wa Lesotho amesema mechi ilikuwa ngumu na kwamba walijiandaa kwa ajili ya kushinda wakijua watakutana na mechi ya aina hiyo lakini imekuwa bahati mbaya kwao kupata sare.
0 comments :
Post a Comment