Klabu ya Everton itatua jijini Dar Julai 13 katika ziara ya kwanza Afrika Mashariki kufanywa na klabu ya Ligi Kuu Uingereza.
Ni ziara maalum kwa ajili ya kucheza mechi na mshindi wa Kombe la SportPesa ambao ndio wadhamini wakuu wa Everton.
Wakati ziara hio ikiwa imeshathibitishwa na pande zote, huenda washambuliaji Romelu Lukaku wa Everton na Wayne Rooney wakabadilisha makazi endapo dili baina ya vilabu vyao likikamilika.
Manchester United wanatajwa kuanza mazungumzo ya kumnunua Lukaku kutoka Everton.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Uingereza, Manchester United wanataka kumnunua Lukaku kwa pesa pamoja na kumtoa Rooney.
Rooney amekiri kuwa endapo atabaki katika Ligi Kuu Uingereza basi ni Everton pekee anayoweza kuichezea kwani ndio timu iliyomuibua.
kama dili hilo likikamilika ndani ya muda mwafaka basi Rooney anaweza ataambatana na kikosi cha Everton kitakachokuja Dar na kuwa nyota mwingine wa timu ya taifa ya Uingereza kutua katika ardhi ya Tanzania ndani ya kipindi cha muda mfupi baada ya David Beckham