Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB, Hamornize leo amkata mzizi wa fitina baada ya kuweka mambo hadharani na kusema kuwa mpenzi wake mpya ni mjamzito hivyo karibu atajifungua.
Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya Ultrasound ikionyesha kichanga kikiwa tumboni na kuandika maneno haya “Mnh! nawaza huu mchanganyiko wa damu ya kimakonde na ya kizungu sijui itatuletea mwana gani… asa nikiona kakomwe hapo, kananistua Chonde mtoto chukua vyote kwangu ila kwenye rangi jitahidi uibe ya mama yako…..!!! nikavimbe Mtwara”
Haya yamekuja ikiwa ni siku chache tu tangu kijana huyo anayetamba na nyimbo kama Show Me, Nambie, Birthday alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, Jackline Wolper.
Lakini mbali na hiyo, alianza kwa kuweka picha ya mrembo mwenye asili ya magharabi na kuandika chini Ujinga ni wakati wa kwenda tu, huku akiongezea na mabusu kibao. Kwa hapo mtu mzima unaunganisha nukta halafu unapata mchoro kamili.
Huu ndio ujumbe alionadika Harmonize usome hapo chini
Huu ndio ujumbe alionadika Harmonize usome hapo chini
0 comments :
Post a Comment