PATRICK Ole Sosopi, makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, akituhumiwa kufanya mkusanyiko usio na kibali.
Sosopi amehifadhiwa mahabusu ya kituo kikuu cha polisi manispaa ya Iringa, baada ya kujisalimisha leo leo Jumatatu kufuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai – mkoa wa Iringa (RCO).
Sosopi aliamriwa kujisalimisha ofisini kwa RCO wa Iringa, ili kuhojiwa, akikabiliwa na tuhuma za kufanya mkusanyiko usio na kibali mnamo tarehe 16 Juni, 2017 katika Kata ya Mlenge, Pawaga Jimbo la Isimani mkoani Iringa.
Jackson Mnyawami, Katibu wa Bavicha mkoa wa Iringa akizungumzia kukamatwa kwa Sosopi amesema, “Tumefanikiwa kukutana na RCO wa Iringa, tunezungumza naye kwa kwa zaidi ya saa moja lakini amesema Sosopi hawezi kupewa dhamana leo.
“RCO amedai kuwa Sosopi ni kiburi, wameshamuonya mara kadhaa lakini anaendelea na mikutano. Amesema lazima wamlaze mahabusu mpaka kesho na kwamba kama tunataka kumdhamini tuende kesho asubuhi.”
Hii ni mara ya tatu kwa jeshi la polisi mkoani Iringa kumkamata Sosopi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi. Juni mwaka jana, lilimkamata na kumsafirisha mpaka jijini Dar es Salaam, akituhumiwa kwa uchochezi, hata hivyo alihojiwa tu, hakufikishwa mahakamani.
Sosopi ni hasimu mkubwa wa kisiasa wa William Lukuvi, Mbunge wa Jimbo la Isimani na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Sosopi alitoa upinzani mkali kwa Lukuvi.

0 comments :
Post a Comment