Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), leo Juni 19, imesema inatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira kwa tuhuma za uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hilo.
Uamuzi huo umetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola, alipozungumza na wanahabari.
Harbinder Singh Sethi na Rugemalira, wanatuhumiwa kuhusika na sakata maarufu la Tegeta Escrow na IPTL, ambapo Kamishna Mlowola, amesema wamelichunguza shauri hilo kwa muda mrefu, na sasa ni muda muafaka wa kuwafikisha mahakamani, wahusika.
“Tulichunguza shauri hili kwa muda mrefu, na sasa umefika wakati muafaka wa kuwafikisha wakuu hawa wa mashauri haya ya uhujumu uchumi wa nchi yetu mahakamani,” alisema Mlowola
Kamishna Mlowola, ametoa wito kwa jamii ya kwamba Serikali ina nia ya dhati ya kupambana na vitendo vya uhujumu uchumi wa nchi ili wananchi wapate maisha bora.
0 comments :
Post a Comment