Mahakama Nchini Uganda Yaamuru Kaburi La Ivan Lifukuliwe

Wanasheria nchini Uganda wameamua kuifikisha familia ya Ivan Mahakamani kwa makosa ya kuzika pesa halali za Jamhuri ya Uganda katika kaburi la ndugu yao Ivan. Kwa nchi yoyote kitendo hicho hakikubaliki kwani pesa hizo zingeweza kutumika katika shughuli zingine na kukuza uchumi wa nchi.

Kitendo hicho kinakuja baada ya marafiki wa Ivan kumwaga mamilioni ya pesa ndani ya kaburi la Ivan kama njia ya kumuaga rafiki yao aliyekuwa maarufu kwa matumizi makubwa ya pesa.

Wanasheria wakiongozwa na Tugume Gideon wa Human Rights Defenders Association Uganda wamesema hawakufurahishwa na kitendo cha RICH GANG cha kuzika mamilioni ya pesa ndani ya kaburi, na kwa vile ni kinyume cha sheria,

wameamua kwenda mahakamani kuomba kaburi la Ivan lifukuliwe, pesa zitolewe zikafanye shughuli nyingine na waliohusika washitakiwe kwa kuharibu kwa makusudi alama ya taifa.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment