Eneo la hospitali ya Kinyonga, ambako mtoto huyo amelazwa
Mwanamke mmoja mkazi wa Kilwa Kivinje, mkoani Lindi, anadaiwa kumchoma moto mwanae wa kumzaa mwenye umri wa miaka tisa, akimtuhumu kumwibia kiasi cha fedha cha Shilingi elfu saba.
Mwanamama huyo aliyetambulika kwa jina la Zabibu Binamu (30), anayejishughulisha na uchuuzi wa samaki, anadaiwa kumfunga mikono yote miwili mtoto huyo na kisha kutekeleza unyama huo.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Kinyonga ambayo ndio hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Dkt. Salehe Aboubakari, amethibitisha kupokewa kwa mtoto huyo na kulazwa tangu Mei 19, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mwandish wa Azam TV, John Kasembe, aliyefika hospitalini hapo, amesema mama huyo aliwekwa ndani kwa siku tatu, japo kwa sasa yupo nje kwa dhamana.
Kwa sasa Zabibu yupo hospitalini Kinyonga, akimuuguza mtoto wake huyo ambaye ni wa pili kati ya watatu alionao.
CHANZO AZAM TVFacebook