IN SUMMARY

Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema jana Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.
Marekani. Serikali nchini Marekani imeanza uchunguzi wa  matukio makubwa ya udukuzi katika mifumo ya kompyuta duniani.
Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema jana Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.
Mashirika mbalimbali zikiwamo taasisi za kifedha, idara za Serikali na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa zilizoathirika.
Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na limeendelea sehemu nyengine duniani ikiwamo Afrika.