IN SUMMARY
Waliopigwa risasi wametajwa kuwa ni mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.
Kibiti. Viongozi wawili wamepigwa risasi katika Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).
Waliopigwa risasi wametajwa kuwa ni mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa tukio hilo.
Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.
Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwamo askari 13 wa polisi.
0 comments :
Post a Comment