NAPE Moses Nnauye, Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, ameitaka serikali kutopuuza hoja na ushauri unaotolewa na wabunge wa upinzani kwani ushauri wao ni muhimu katika kubainisha mapungufu ya utendaji wa serikali.
Nape pia alikuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali 2017/2018, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa serikali kutopuuza maoni ya kila mbunge kwani yana umuhimu wake.
“Kelele zisiturudishe nyuma, lazima tusonge mbele kwa sababu vita hii ni takatifu, lakini tusipuuze katika kelele nyingi kunaweza kukawa na ushauri mzuri ndani yake.
“Kelele zisiturudishe nyuma, lazima tusonge mbele kwa sababu vita hii ni takatifu, lakini tusipuuze katika kelele nyingi kunaweza kukawa na ushauri mzuri ndani yake.
“Tupuuze wapinzani nadhani, hii vita ni ya kwetu wote, nchi hii ikifaidika na jambo hili ni la kwetu wote bila kujali itikadi za vyama, sasa tusitoboane macho, tusitupiane vijembe visivyo na sababu. Ni wakati wa kuileta nchi yetu pamoja, tukapigane vita na tuishinde,” amesema Nape.
Nape amesema mshikamano wa kitaifa ni muhimu badala ya nyufa za mpasuko kwa misingi ya itikadi za vyama vya siasa ambavyo si muhimu kuliko maslahi ya Taifa.
“Wapinzani na CCM na wengine wote ni vizuri tukaungana kama vita yeyote ama safari yeyote inaweza kuwa na mashimo na mabonde na kunaweza kuwa gharama na vita hii tukubali kuzilipa faida yake ni kubwa,” amesema Nape.
Katika hatua nyingine Nape amesema Rais Magufuli si wa kwanza kuendesha vita ya kutetea rasilimali za Taifa na hivyo si vyema baadhi ya wana CCM kuwabeza marais waliopita kana kwamba wao hawakuwahi kufanya chochote cha kulinufaisha Taifa.
0 comments :
Post a Comment