Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha Marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu (makinikia) kwani katika ripoti zote mbili hakuna sehemu ambayo imewataja wastaafu kuhusika.
Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzia serikali iache kufatilia sakata hilo.
“Viongozi wetu hawajawai kuwa mawakala wa wale wanao tuibia, mawakala tumewabaini ni wale wanao watetea wezi,” alisema Waziri Nchemba.
Waziri Mwigulu ameongeza kusema sifa ambayo inafanya viongozi walioko madarakani wasing’ang’anie madaraka ni viongozi wastaafu kuheshimiwa baada ya muda wa uongozi.
Waziri Mwigulu ameyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa ya Ndago katika mwendelezo wa ziara jimbo kwake Iramba Magharibi kuongea na wananchi kuwaeleza alipofikia kuhusu ahadi ambazo walikubaliana kutekeleza hasa suala la umeme kutokufika katika vijiji vingi akieleza kuwa sababu ni mkandarasi aliyekuwepo mkoa wa Singida aliyetolewa baada ya kushindwa kazi lakini sasa ameambiwa na watu wa wizara ya nishati kuwa wakandarasi wawili wameshapatikana hivyo kuanzia sasa zoezi la kuunganisha umeme vijijini utaendelea kwa kasi hasa wa REA awamu ya Tatu.
Kuhusu ujenzi wa zahanati amesema mpaka sasa zahanati katika vijiji vingi alipopita zimefika hatua nzuri ya kupaua na kuwahidi kuwa pelekea mabati na mbao na mifuko ya saruji 100 ili zahanati hizo zikamilike na kuanza kutoa huduma mapema sana.Facebook