Arsenal wapo katika nafasi nzuri kumsajili nyota wa Barcelona ingawa miamba hao wa Camp Nou wanatamani kumsajili Bellerin
Habari yenyewe ipoje?
Arda Turan amefikia makubaliano na Arsenal kwa mujibu wa habari kutoka Hispania. The Sun limedai kuwa Barcelona wapo tayari kumruhusu Mturuki huyo kujiunga na Washika Mtutu wa London majira ya joto.
Klabu hizo bado hazijafikia makubaliano ya ada ya uhamisho majira ya joto, lakini Arsenal tayari wameshafikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid. Barcelona wanamtaka Hector Bellerin kutoka Arsenal, na hiyo ndiyo sababu kubwa wapo tayari kumruhusu Turan.
Kama ulikuwa hujui…
Hii si mara ya kwanza Arsenal kufikia makubaliano na Turan. Gunners walifanya mazungumzo naye na kutoa ofa kwa Atletico Madrid pia 2015.
Hata hivyo, Barcelona walifanikiwa kumsajili dakika za mwisho na Mturuki huyo akatua Camp Nou.
Luis Enrique alikuwa anataka kuendelea kuwa naye klabuni na alikataa kumuuza. Ernesto Valverde hana mpango wa kubaki naye Camp Nou na yupo tayari kumuuza.
Habari kamili…
Habari zinadai kuwa Arsenal tayari wameshaonana na wakala wa kiungo huyo, Ahmet Bulut, na wamekuwa katika mazungumzo mwezi uliopita.
Barcelona wanataka kitita cha euro milioni 30 kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo, lakini Gunners wapo tayari kulipa euro milioni 25. Wenger anajaribu kupunguza bei hiyo na anataka kufanya mazungumzo mwenyewe.
Arsenal wanamwelekeo wa kufanikiwa katika mazungumzo hayo kwani Barcelona wanataka kumuuza haraka iwezekanavyo. Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Robert Fernandez tayari yupo sokoni kutafuta mrithi wa Arda kwa mujibu wa habari.
Turan alisaini mkataba wa miaka mitano alipotua Barca kutokea Atletico Madrid kwa ada ya euro milioni 34. Bado amebakiwa na mika mitatu kwenye mkataba wake, lakini klabu ipo tayari kumwachilia kwa hasara ya euro milioni 4.
Tofauti na Arsenal, Inter Milan na Galatasaray pia zinataka kumsajili mshambuliaji huyo.
Kifuatacho?