Kiongozi mkuu wa Kanisa la Katoliki nchini Nigeria ameieleza Africa Live, kuwa Papa Francis amekasirishwa sana na kitendo cha makasisi wa dayosisi ya Ahiara iliyopo kusini mashariki mwa nchi hiyo kwa kukataa uteuzi wa askofu wao.
Rais wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nigeria, Askofu mkuu, Ignatius Kaigama,aliyekuwa katika mkutano mjini Rome amesema, Papa Francis ametoa siku 30 kwa makasisi hao kuonyesha utii au wakabiliane na adhabu ya kusimamishwa utumishi wao.
“Niliona maumivu ya Papa machoni mwake. Alikasirika kwa sababu watoto wake wanaenda njia tofauti.”
Askafu Mkuu huyo amesema, Utii kwa Papa ndicho kigezo kikuu kwa kanisa Katoliki kufanya kazi zake:
“Kanisa Katoliki limekuwa na mfumo wake unaofanya kazi kwa miaka zaidi ya mia moja na hilo haliwezi kubadilika sasa kwa sababu wanahitaji watu wao kutoka eneo fulani.
“Kanisa Katoliki limekuwa na mfumo wake unaofanya kazi kwa miaka zaidi ya mia moja na hilo haliwezi kubadilika sasa kwa sababu wanahitaji watu wao kutoka eneo fulani.
“Tumeshikwa na mshangao, hofu na kukatishwa tamaa kwa kukataa uteuzi huo kutoka kwa Baba Mtakatifu.
Askofu mkuu huyo, Kaigama pia amesema, amekuwa akijaribu sana kuwashawishi makasisi hao wa Ahiara kumkubali askofu wao huyo Peter Okpaleke, aliyeteuiwa tangu 2012 ikiwa ni zaidi ya miaka minne na nusu lakini bila mafanikio.

0 comments :
Post a Comment