ANGALIA RATIBA KWA KUBONYEZA LINK ZILIZOPO CHINI KABISA YA POSTI
Mtihani wa kidato cha nne unaanza jumatatu tarehe 10 oktoba hadi novemba 17 2017
mtihani wa kidato cha pili unaanza tarehe 13 novemba hadi 24 novemba
mtihani wa darasa la saba unaanza tarehe 6 hadi 7 septemba
mtihani wa darasa la nne unaanza tarehe 22 hadi 23 november
MAELEKEZO MUHIMU KWA MTAHINIWA
  1. Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2017 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
  2. Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya mtihani, hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.
  3. Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Mtihani na Ratiba ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.
  4. Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa mtihani wa Kiswahili, English Language, Maarifa ya Jamii na Sayansi.
  5. Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa mtihani wa Hisabati.
  6. Msimamizi wa watahiniwa WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.
  7. Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za mtihani na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
  8. Karatasi zenye majibu ya watahiniwa wenye UONI HAFIFU zifungwe kwenye bahasha za pekee. Zisichanganywe na karatasi za watahiniwa wenye Uoni wa kawaida.

ZAMBAZA KWA MARAFIKI KADIRI UWEZAVYO