Raynavvy Ashinda Tuzo BET

Hatimaye kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikiwa kunyakua tuzo ya BET.

Tuzo hizo ambazo zimegaiwa usiku huu mjini Los Angeles, katika ukumbi wa Microsoft Theater Centre, Rayvanny ambaye alikuwa akiwania tuzo hizo kupitia kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act amefanikiwa kuibuka kidedea.

Wasanii wengine ambao alikuwa akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica).


Baada ya kushinda tuzo hiyo, Ray kupitia mtandao wake wa Instagram ameshukuru kwa kuandika, “God is good all the time.Asante Mungu wangu Ulieniumba,Unaejua mwanzo na mwisho wangu.Uliyaona machozi yangu nilipokua mpweke sina furaha na mwenye majonzi mengi.WEWE NDIYE MUWEZA…”

“Asanteni wadau Wote mlio VOTE kwa Ajili yangu Ushindi umerudi Nyumbani.SITOACHA KUSHUKURU UONGOZI MZIMA #WCB @babutale @sallam_sk @Diamondplatnumz @mkubwafellatmk @kameboy_j @ricardomomo thanks Alot @bet_intl @betawards @bet_africa #WCBFORLIFE MAMA I LOVE YOU,” ameongeza
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment