Ronaldo aweka historia mpya Urusi

Ronaldo jana katika ushindi wa 4-0 dhidi ya New Zealand alifunga goli lake la 75 kwa timu yake ya taifa na kuonesha kiwango cha hali ya juu kilichomfanya kuandika historia ya mchezaji pekee kuchagulia mchezaji bora wa mechi mara tatu mfululizo katika michuano hiyo pia timu yake ya taifa.
Akihojiwa na waandishi wa habari baada mchezo huo, Ronaldo alionesha hisia kali kwa kuguswa na tukio hilo;
” nina furaha ya ajabu kuwa sehemu ya ushindi huu unaoiwezesha timu yetu kuingia hatua ya nusu fainali. Ni jambo zito sana kwangu pia kwa wenzangu na nchi yangu . Tumejipanga kufanya kile ambacho Mungu alituwezesha nchini Ufaransa”
Ureno ni mabingwa wa kombe la Euro mwaka 2016 hivyo wakifanikiwa kuchukua kombe hili la mabara watakuwa wamejiwekea historia kubwa duniani na bara la Ulaya na Ronaldo kama nahodha kuzidi kuimarisha rekodi zake na timu yake ya taifa.
Mexico pia wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwaondoa wenyeji Urusi katika
michuano hiyo jijini Kazan kwa ushindi wa goli 2-1
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment