Baada ya kutangaza kuwa yeye ni baba wa watoto mapacha, staa wa soka kutoka Ureno Cristiano Ronaldo amepost picha ya mapacha wake inasemekana mapacha hao ni wa kike na kiume.
Cristiano Ronaldo jana alikumbwa na simanzi kubwa baada ya timu hiyo kutupwa nje ya kombe la mabara na Chile, lakini huenda simanzi hiyo imepotea baada ya kukutana na watoto wake mapacha.
Ronaldo alichapishwa habari kuhusu yeye kuwa baba wa machapa muda mfupi baada ya Ureno kutolewa katika michuano hiyo inayoendelea nchini Urusi.
Wiki kadhaa zilizopita iliyopita kulikuwa na tetesi za kuwepo kwa mwanamke mmoja ambaye hajulikani ni nani lakini alikuwa na mimba ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, jambo hilo limekuwa siri kubwa katika familia ya Ronaldo lakini hadi mama yake mzazi analijua hilo.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana mpenzi mpya Georgina Rodriguez inasemekana mwanamke ambaye amezaaa naye ni mwenyeji wa bara la America na hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanasoka huyu kuzaa na mwanamke asiyejulikana kwani hata mtoto aliyenaye mama yake hajulikani.
Sasa leo kupitia ukurasa wa twitter wa Cristiano Ronaldo amepiga picha akiwa na watoto wake hao mapacha na kusema kuwa>>So happy to be able to hold the two new loves of my life 🙏❤