Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linawashikilia watu watatu kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto aina ya SMG, yenye namba za usajili 197705975, kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei, amewataja watu hao kuwa ni Juma Lauka (39) mkazi wa Mvugwe Kigoma, Hussein Ulanga (40) mkazi wa Mang’ula na Hashim Mohamed (45) ambaye pia ni mkazi wa Mang’ula.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Azam TV, Robert Mayungu aliyeko mkoani Morogoro, watuhumiwa wote watatu wanatajwa kuwa vinara wa matukio ya ujangili
Watuhumiwa hao walikamatwa katika Kitongoji cha Minazini, kilichoko Kata ya Mang’ula wilayani Kilombero mkoani Morogoro kutokana na ushirikiano wa maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA)