Serikali imetoa kibali cha ajira 15,000 ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kumiliki vyeti vya kughushi.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu nafasi hizo zitajazwa.
Mh.Kairuki amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati aijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya ujazwaji wa nafasi hizo ambaye amekiri upungufu huo kusababisha usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia wananchi na kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.
0 comments :
Post a Comment