Moses Kitandu, Try Again, na Tshabalala wakipokea tuzo
Klabu ya Simba imempatia cheti cha heshima mmoja wa wafadhili wakubwa wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘Mo’ katika kutambua na kuthamini mchango wake katika mafanikio iliyopata msimu wa 2016/17.
Cheti hicho kimekabidhiwa kwa Salim Muhene ‘Try Again’ kwa niaba ya Mo katika hafla ya futari iliyofanyika usiku wa jana Jijini Dar es Salaam
Hafla hiyo iliyoambatana na utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora wa timu hiyo kwa msimu uliopita, ilishuhudia beki wa kushoto Mohamed Hussein akilamba tuzo nyingine kwa kuibuka mchezaji bora wa msimu kwa klabu ya Simba.
Tuzo hiyo inamfanya nyota huyo maarufu kwa jina la Tshabalala kuwa ametia kibindoni tuzo mbili za mchezaji bora wa msimu, akiwa ametoka kutwaa tuzo kama hiyo kama mchezaji bora wa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara katika tuzo zilizotolewa na wadhamini ambao ni Vodacom Tanzania.
Tshabalala pia ndiye aliyeibuka kuwa mchezaji bora wa klabu ya Simba na wa ligi kwa ujumla kwa Mwezi April.
Tuzo nyingine usiku wa jana imekwenda kwa Moses Kitandu aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa klabu ya Simba.Facebook