Magufuli amemshahuri asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake katika kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi” amesema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Anna Mghwira, amemshukuru Rais Magufuli, kwa kumteua kuwa mkuu wa mkoa na kusema kuwa anaamini kuwa hakuna upinzani usiyopenda maendeleo na yeye si mpinzani wa maendeleo.
0 comments :
Post a Comment