TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA VYUO VYA SERIKALI NA VISIVYO VYA SERIKALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuandaa walimu ni kuhakikisha kuwa wanaojiunga na Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada ni wenye sifa stahiki.
Kwa kuzingatia hilo, waombaji wa mafunzo haya ni wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu katika mtihani wa kuhitimu kidato cha NNE (kwa waombaji wa Astashahada) na SITA (kwa stashahada).
Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati, kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo haya. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza nafasiza Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada naStashahada kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Masomo yataanza mwezi Septemba, 2017. Kwa waombaji wa programu za Ualimu katika vyuo vya Serikali watatakiwa kuomba kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) (www.nacte.go.tz) kwa kubofya kwenye ‘ Apply online (NOAVS)’ kisha kufuata maelekezo.
Kwa waombaji kwenye vyuo visivyo vya serikali watatakiwa kuomba moja kwa moja kwenye vyuo husika. Vyuo visivyo vya serikali vitadahili na kufanya uchaguzi wa wanafunzi wenye sifa na kisha kuwasilisha NACTE majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuyatangaza.
Vyuo vinaelekezwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa mwaka wa masomo 2017/2018 uliotolewa na NACTE.
Aidha, Sifa za kujiunga na programu mbalimbali za Ualimu kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali ni kama zilivyoanishwa katika tangazo hili na kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili (Admission Guidebook) kilichopo hapo chini soma vizuri ndipo utume maombi ya kozi husika