Wenger Apewa Pesa Za Usajili


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anafahamika kwa ubahili, amepewa kitita kikubwa cha fedha akiambiwa azitumie kufanya usajili wa wachezaji wapya.

Mabosi wa klabu hiyo wamemtengea kocha huyo Mfaransa Pauni 165 milioni na kumweleza azitumie kuimarisha kikosi chake.

Bodi ya klabu hiyo imempa kitita hicho kikubwa cha fedha ili kumwezesha kushindana na wababe wengine England kwenye soko la usajili.

Tayari, Wenger anayo majina ya Riyad Mahrez wa Leicester City na Mturuki Arda Turan ambaye ameachwa na Barcelona.

Wenger ameambiwa awe makini na kikosi chake Arsenal msimu ujao kwani mwisho wa msimu atatakiwa kutwaa taji ambalo amelikosa tangu msimu wa 2004.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment