Balozi Juma Mwapachu amestaafu kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya madini ya Acacia baada ya uteuzi wake wa miaka mitatu kumalizika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, balozi Mwapachu ambaye alikuwa mkurugenzi asiye na mamlaka ya kiutendaji ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi Julai 13.
Kampuni hiyo imeridhia uamuzi wa balozi Mwapachu na kumtakia kila la heri katika shughuli zake zingine.
Hatua hiyo ya Mwapachu inakuja ikiwa imepita miezi kadhaa mara baada ya kuzuka kwa sakata la mchanga wa dhahabu (Makinikia), ambapo Kampuni ya Acacia ilidaiwa kuusafirisha kwenda nje ya nchi kinyume na sheria, na hivyo Serikali ya Tanzania kuamua kuzuia usafirishaji huo kwa kusema inapoteza mapato yake.
Kwa sasa, Serikali na kampuni ya Acacia inayomilikiwa na Barrick Gold Corporation, zinajiandaa na mazungumzo ili kuangalia ni kwa namna gani Serikali italipwa fedha zake zilizopotea kutokana na usafirishaji huo wa makinikia.
Hivi karibuni, Serikali ya Tanzania ilisema kuwa Mwenyekiti wa kampuni ya Barrick, Profesa John Thornton alikubali kulipa fedha hizo ambazo ni zaidi ya takribani trilioni 100