China imepiga Marufuku matumizi Ya mtandao Wa whatsApp

Related image


Na Karim-0658303252
Wale wazee wa Kuchat,Kama una safari ya kwenda nchini China unatakiwa ujiandae kisaikolojia. Hii ni kutokana kwamba mitandao muhimu ambayo uliizoe kutumia ukiwa Tanzania ukiingia nchini China hutaweza kuitumia.

Serikali ya China imepiga marufuku matumizi ya Mtandao wa WhatsApp.Huu nimuendelezo wa nchi hiyo kuipiga marufuku mitandao yote yenye ubia na Mtandao wa Google.

Kabla ya WhatsApp tayari nchi hiyo ilishazuia matumizi ya mitandao ya Facebook,Twitter,Instagram na mitandao yote inayoshabihiana na mtandao wa Google ikiwemo Youtube.

Tafiti za kiintelijensia zimebaini kuwa China wanazuia matumizi ya mitandao hiyo kwa sababu ni mitandao inayomilikiwa na wamarekani,na ukiangalia uhusiano kati ya China na marekani haupo sawa.

Mtandao pekee unaoweza kutumia bila shida ukiwa China ni Wechat.

Ili uweze kutumia mitandao hii yaani WhatsApp,Twitter,Instagram,Facebook na Google unatakiwa kuwa na VPN (Virtual Private Network) kwenye "device" yako.

Angalia video hii hapa chini ikimuonsha  Mwafrika aliyezoea kutumia mtandao wa WhatsApp akiwa China akilalamika baada ya WhatsApp kufungiwa chini  humo (China).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment