Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya tuhuma zinazomkabili za kutoa kauli za uchochezi alipokuwa akiongoza kikao cha Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amesomewa shtaka moja la kumtukana Rais John Magufuli katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mdee alisomewa kosa hilo mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa na wakili wa serikali Nassoro Katuga ambapo imeelezwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.
Katuga alidai kuwa July 3, 2017 katika Ofisi za Chadema makao makuu, alimtukana Rais Magufuli kwa kumwambia ” Anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afunge break,”. Baada ya kusomewa kosa hilo, Mdee alikana kosa.Wakili Katuga alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika anaomba kesi iahirishwe.
Mdee amedhaminiwa kwa bondi ya shilingi milioni kumi na wadhamini wawili. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu.Faceboo