Winga Shiza Kichuya anachuana na Mzimbabwe, Ovidy Karuru kuwania ufungaji bora wa michuano ya COSAFA.
Kichuya ana magoli mawili hadi sasa sawa na Karuru anayechezea AmaZulu ya Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.
Tayari Tanzania imefuzu Robo Fainali baada ya kuongoza Kundi A na itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini Jumapili ya kesho saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace.
Mbali na Kichuya na Ovidy Karuru kuwa na mabao mawili kila mmoja, wengine waliofanikiwa kufunga bao moja kila mmoja hadi sasa ni;
Blessing Majarira (Zimbabwe)
Roddy Melanie (Shelisheli)
Ocean Mushure (Zimbabwe)
Saimon Msuva (Tanzania)
Mutong (Msumbiji)
Augusto Quibeto (Angola)
Joseph Perticots (Mauritius)
Rinjala Raherinaivo (Madagascar)
Ardino Raveloarisona (Madagascar)
Stelio (Msumbiji)