Kipa bora wa COSAFA, atua Msimbazi


Klabu ya Simba imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili kipa Said Mohammed ‘Nduda’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Nduda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi, kabla ya kusafiri na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars leo kwenda Rwanda.
Huyo ni kipa wa pili wa Taifa Stars baada ya Aishi Salum Manula ambaye pia amesajiliwa Simba SC kutoka Azam FC dirisha hili la usajili.
Maamuzi ya Simba kumsjili kipa huyo wa zamani wa Yanga SC, yamekuja baada ya kuchaguliwa kuwa kipa bora wa michuano ya Kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini mwezi uliopita licha ya kudaka mechi moja pekee ya kusaka mshindi wa tatu, akimpiku Manula aliyedaka mechi zote tano zilizotanguliwa.
Nduda anakwenda kukamilisha idadi ya makipa watatu Simba baada ya Manula na Emmanuel Mseja aliyesajiliwa kutoka Mbao FC baada ya klabu hiyo kuwatema makipa wake wote iliyokuwa nao msimu uliopita ambao ni Daniel Agyei, Peter Manyika Junior na Dennis Richard.
Ikumbukwe kuwa Mei 6 mwaka 2012 ni Simba SC iliyomponza Nduda kufukuzwa Yanga SC baada ya kumfunga mabao manne ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili, katika mchezo wa marudiano wa ligi kuu ya Tanzania Bara, ambao wekundu hao wa Msimbazi wakishinda 5-0.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment