Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, amekanusha taarifa zinazodai kuwa serikali imefuta mafunzo kwa watumishi wa umma.
Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 19, kwenye kikao kazi na watumishi wa umma wa halmashauri ya manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
Kairuki amezielekeza taasisi za serikali kuandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Kiongozi huyo amesema mwajiri anapoandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi wake, ni vyema mpango huo ukawashirikishi kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake.
Kairiku amesema miongoni mwa sehemu ya mpangilio huo ni pamoja na na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa.
“Napokea malalamiko mengi kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae mpango wa mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,” alisema kiongozi huyo.


0 comments :
Post a Comment