Dar es Salaam. Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Azam, Fatna Ramole amepatikana ikiwa ni saa 48 baada ya kudaiwa kutoweka.
Ndugu yake, Lulu Ramole amezungumza na Mwananchi leo (Julai mosi) na kueleza kuwa kwa sasa yeye na Fatna wapo kituo cha Polisi, Kinondoni.
Lulu aliandika katika ukurasa wake wa twitter leo saa nane mchana akiwashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompa hadi dada yake kupatikana.
“Msamaria alitupigia simu amepatikana Makongo, nipo naye lakini siwezi kueleza kwa undani alivyopatikana, uchunguzi unaendelea,” amejibu kwa kifupi Lulu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amethibitisha kupatikana kwa Fatna, lakini kwa maelezo na ufafanuzi zaidi alishauri familia ya mwanahabari huyo iulizwe.
“Lakini tutawaita hapa kwa mahojiano zaidi,” amesema
0 comments :
Post a Comment