Waliomdhalilisha mwanamke ndani ya basi wahukumiwa kifo


Wanaume watatu waliomshambulia na kumdhalilisha mwanamke mmoja ndani ya basi nchini Kenya wamehukumiwa kunyongwa na hakimu wa mahakama ya mjini mkuu wa Nairobi, Kenya. Tukio hilo linadaiwa lilitokea usiku wa Septeamba 19, 2014.
Gazeti la Star limeripoti kuwa,watatu hao walipatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia nguvu. Shtka ala kumvua nguo mwanamke huyo kiliwapatia hukumu ya miaka 25 ambayo iliathiriwa na adhabu ya kifo.
Wanaume hao watatu ambao ni dereva, kondakta wake na mtu mmoja wanadaiwa mwaka 2014 walimpora na kumdhalilisha mwanamke huyo ndani ya basi alilopanda, kitendo ambacho hukumu hiyo imekielezea kama ‘Kitendo kisichofaa na kisicho na maana, kwa mantiki ya kufuwafurahisha wao kwa sababu ya kumvua nguo mwanamke huyo.’
“Kile ambacho mlidhani ni utani hakiwezi kuchukuliwa kwa wepesi kwani faragha ya mwanamke na adabu yake vinahitajika kuheshimiwa wakati wote,” alisisitiza Hakimu Francis Andayi.
Kielelezo pekee katika mashtaka hayo kilikuwa ni video iliyosambazwa kama kirusi. Kipande hicho cha video cha sekunde 59 kiliamsha taharuki katika nchi hiyo ya Afrika mashariki kwa kusababisha wanawake na watoto kuandamana wakidai haki.
Mwanamke huyo aliyedaiwa kudhalilishwa kutokana na madai ya mavazi aliyokuwa amevaa, ameiambia mahakama kuwa tukio hilo lilitokea kwa zaidi ya muda unaoonyeshwa katika video hiyo. Ameiambia mahakama wakati wa kesi hiyo kuwa, ilimbidi aseme uongo kuhusu yeye kuwa mwathirika wa HIV kwaajili ya kujinusuru na kubakwa.
Tukio hilo lilitokea katika kituo cha kujaza mafuta cha Millennium huko Githurai 44, kaunti ya Nairobi, ambapo pia wahalifu hao walimpora mwanamke huyo fedha taslimu shilingi za Kenya 41,700 (sawa na dola 400
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment