Chidi benzi Ni Mkali Sina shaka Na uwezi Wake.....Dudubaya

Msanii mkongwe wa bongo fleva Dudubaya ameanza kujirudi na kumsifia rapa mwenzake Chid Benz kwa kuweza kukabiliana na hali aliyokuwa nayo awali ya matumizi ya dawa za kulevya.
Dudubaya ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kukutana na Chid katika 'show' mbalimbali akiwa anaimba kwa uwezo wa juu zaidi jambo ambalo likamfanya amini kwamba rafiki yake ameamua kuachana na vitu ambavyo vilimsababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo pamoja na kazi zake kisanaa kwa ujumla.
"Suala la msingi kwa sasa nampa 'big up' Chid Benz kwa kuwa ameweza ku-recover katika hali yake, pia namsifu kwa kuweza kuitumia 'mic'  vizuri na pumzi ya kutosha. Sina mashaka naye, namkubali sana ila mimi kama kaka yake namsisitizia tena, sitaki nimemuone anarudi kule alipokuwa ameangukia, Mungu amuinuie na amsimamie", amesema Dudubaya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment